Wednesday, 26 April 2017

MAWASILIANO.


MAWASILIANO.SIMU NO. +255 713 684 712
E-MAIL: healthylivingproduct6@gmail.com
TUPO : KUNDUCHI BAHARI BEACH

UWEZO ASILIA WA MWILI KUJILINDA NA KUJITIBU


Mwili wa binadamu unafanya mambo mengi ya kibaiolojia ambayo mara nyingi ni vigumu kuyaelewa.
Mwili una mifumo mbalimbali ya ulinzi ambayo inatulinda na hatari zinazoweza kutudhuru. Mifumo hiyo inatulinda masaa 24 ya siku, Siku zote 7 za wiki, katika mambo yote yanayoweza kuhatarisha maisha yetu.
Yafuatayo ni mambo yanayofanywa na mwili ambayo ni kati ya hiyo mifumo ya ulinzi wa mwili wa binadamu.
kwa kawaida mfumo wa ulinzi unapaswa kuwa wa uwiano wa kawaida ili kuleta ufanisi ,hii ina maanisha kuwa iwapo mfumo huu utakuwa dhaifu basi magonjwa yatashambulia mwili kupitia bacteria,fangasi au virusi hali kadhalika mfumo huu ukiwa na nguvu kupita kiasi pia huleta madhara kama ya allergy(mzio) na arthritis ambapo kinga hushambulia seli za mwili wenyewe(auto immune diseases) hivyo mfumo wa ulinzi umegawanyika katika sehemu tatu;
Ulinzi wa kiumbo(mechanical barrier)-mfano i.e ngozi hulinda kwa kufunika viungo vya mwili dhidi ya maadui wa nje ya mwili,pia kupitia ngozi bacteria wazuri wasio na madhara hukaa.Nyusi katika pua hulinda mfumo wa hewa kwa kudaka uchafu 
ULINZI WA KIBAOLOJIA-BACTERIA WAZURI(normal flora) huishi katika ngozi na ndani ya mfumo wa lishe kuzuia bacteria wabaya(pathogens) wasishambulie mwili
ulinzi wa kikemikali(chemical barrier);.ASIDI TUMBONI
Ndani ya tumbo kuna tindikali asilia yenye uwezo wa kuua bacteria wasio wazuri wanaovamia mfumo wa lishe,tindikali hii hujulikana kama hydrochloric acid,huweka mazingira mazuri ya kazi kwa vichocheo vya usagaji(enzymes)   wa vyakula vya protein.Tindikali hii ikizidi huleta madhara ya vidonda vya tumbo
Machozi machoni (TEARS)huwa na kemikali ijulikanayo kama lysosomes ambayo huangamiza wadudu germs iwapo jicho litachafuliwa
MATE(SALIVA) nayo huwa na kemikali ya kuua bacteria wabaya wasilete madhara mdomoni namfumo wa lishe kiujumla  na ,iwapo mate yatakauka mdomoni ,bacteria wabaya huzalishwa na kusababisha harufu mbaya(halitosis)
MENGINEYO;

1. KUPIGA MIAYO (YAWNING)
Lengo kubwa la kupiga muayo ni kuupoza ubongo baada ya joto kuzidi kwenye ubongo au baada ya ubongo kuchoka kufanya kazi.
Vile vile kama ukiwa umechoka au una njaa husabababisha oxygen kupungua kwenye damu na kwenye mapafu, hii hupelekea tatizo la kupumua, hivyo kupiga miayo husaidia kuingiza oxygen ya ziada mwilini ili irudishe mwili katika hali yake ya kawaida.
2. KUPIGA CHAFYA (SNEEZING)
Mara nyingi tunapiga chafya pale pua zetu zinapokua zimejaa bakteria wa magonjwa ambao hawahitajiki mwilini, Vumbi pamoja na takataka mbali mbali zilizoingia kupitia pua.
Hivyo kupiga chafya ni kitenda cha mwili kujisafisha kwa kuyatoa hayo matakataka nje yaliyoingia mwilini.
3. KUJINYOOSHA (STRETCHING)
Kuninyoosha mwili ni kitendo kisicho cha hiari ambacho lengo lake ni kuuandaa mwili kwa ajili ya kazi mbalimbali za kutumia nguvu utakazokabiliana nazo kwa siku nzima. Lakini pia kujinyoosha kunaipa misuli ya mwili mazoezi na kuiweka sawa vilevile kunarudisha mzunguko wa damu katika hali yake ya kawaida na kumtoa mtu katika uchovu.
4. KWIKWI (HICCUPING)
Najua umewahi kupata kwikwi, na mara nyingi mara baada ya kumaliza kula chakula. Je umeshawahi kujiuliza ile sauti ya ajabu ya kwikwi inasababishwa na nini au kwa sabababu gani watu hushikwa na kwikwi?
Hiyo yote husababishwa na DIAPHRAGM (tamka DAYA - FRAM) kiungo kinachopatikana ndani ya mwili wa binadamu chini kabisa ya kifua baada ya mapafu(lungs). Kazi kubwa ya diaphragm ni kusaidia katika upumuaji, (inhale) na (exhale). Pale unapoingiza hewa ndani (inhale) diaphragm hushuka chini ili kusaidia kuivuta hewa ifike kwenye mapafu. Na unapotoa hewa nje (exhale) diaphragm hutulia kwa kubakia sehem yake ili kuwezesha hewa chafu kutoka nje kupitia pua na mdomo.
Sasa basi, kuna wakati diaphragm kubugudhiwa na kuisababisha kushuka chini kwa kasi sana jambo linalosababisha wewe kuvuta hewa (inhale) kwa kasi isiyo ya kawaida kupitia koromeo la sauti, hewa ikifika kwenye box la sauti (larynx), sehem hiyo hujifunga kwa haraka sana ili kuzuia hewa isipite huko na ndipo KWIKWI hutokea.
Mambo mengine yanayoweza kuibugudhi diaphragm na kuisababisha kufanya kazi vibaya mpaka kupelekea kwikwi ni kitendo cha kula haraka haraka au kuvimbewa.
5. KUJIKUNJA KWA NGOZI YA VIDOLE VYA MIKONO BAADA YA KULOWA AU KUKAA MUDA MREFU KWENYE MAJI.
Je umewahi shuhudia jinsi ngozi ya vidole vyako inavyojikunja baada ya kufua nguo muda mrefu au kushika maji muda mrefu? Unajua ni kwa sababu gani ngozi hujikunja kama ya mtu aliyezeeka angali yu kijana mara baada ya kukaa sana kwenye maji?
Watu wengi kabla walizani kwamba kujikunja kwa ngozi hiyo hutokana na maji kuingia kwenye ngozi na hivyo ngozi hujikunja baada ya kulowa.
Lakini wanasayansi baada ya kufanya utafiti kwa muda merefu juu ya nini hasa hupelekea ngozi kujikunja? Walisema HAPANA si kwa sababu ya ngozi kulowana. Na walikuja na majibu haya.
Mwili unapokutana na majimaji mara moja hupeleka taarifa na kutafsiri kwamba mazingira hayo yana UTELEZI (Slippery) hivyo kutasababisha mikono kushindwa kushika (Grip) au kukamata vitu kwa urahisi kutokana na utelezi huo. Hapo mwili huchukua hatua ya haraka kuikunja ngozi ya mikono yako ili kurahisisha ushikaji wa vitu vinavyoteleza ndani ya maji pamoja na kutembea kwenye utelezi.
6. VIPELE VIPELE VYA BARIDI KWENYE NGOZI (GOOSEBUMPS)
Kazi kubwa ya vipele hivi ni kupunguza kiasi cha joto la mwili linalopotea kupitia matundu ya ngozi. Hivyo kwa kufanya hivi humfanya binadamu kutunza joto la mwili hata katika mazingira ambayo hali yake ya hewa si rafiki kwa mwili wa mwanadamu au ni yenye baridi sana.
7. MACHOZI (TEARS)
Zaidi ya kuwa majimaji (MUCOUS MEMBRANE ) yanayopatikana kwenye Macho ambayo kazi zake ni kulilinda jicho dhidi ya kitu chochote kigeni kinachoingia jichoni (mfano unapokata vitunguu au mdudu anapoingia jichoni huwa unatoa machozi mengi eeeh!! Pia dhidi ya upepo na moshi) na pia hutumika kama kilainishi cha jicho pale linapokuwa linazunguka zunguka (blink).
Vilevile machozi yana kazi ya kupunguza HISIA ZA HUDHUNI zinazozalishwa mwilini. Wanasayansi wanaamini kuwa mtu anapokua mwenye msongo wa mawazo (stress) mwili hutengeneza kitu kipya ili kwenda kubugudhi na kuharibu maumivu yote ambayo mtu anajisikia. Hivyo machozi yanayozalishwa hapa huwa na kemikali na yanafahamika kama NATURAL PAINKILLER. Machozi haya ni tofauti na machozi ya kawaida, lengo lake hasa la kuzalishwa ni kwa ajili ya kuondoa kabisa maumivu yaliyozalishwa mwilini
Hivyo mpaka hapa tumeona kua kuna machozi ya aina tatu ambayo ni
i. Basal tears (vilainishi)
ii. Reflex tears (mlinzi)
iii. Emotion tears (mtuliza maumivu)
8. KUSHTUKA USINGIZINI (MYOCLONIC JERKS or HYPNIC JERK).
Je! Ushawahi kutokewa na hali hii? umelala halafu ghafla unashtuka usingizini kwa mguvu nyingi kama umepigwa na shoti ya umeme na akili inakurudi ghafla huku mapigo ya moyo yakikuenda mbio? Na hali hii ikakutokea pasipo hata kuota ndoto yoyote?
Basi usiogope au kuwasingizia watu uchawi, hii ni hali ya sayansi ya mwili.na ni njia moja wapo katika ile mifumo ya mwili kujilinda.
Je hutokeaje?
Hii ni hali ya ajabu sana isiyofanywa kwa hiari ambayo huwatokea watu mara tu wamejinyoosha kitandani na kupitiwa na usingizi, mwili hutetemeshwa na kusukumwa kwa nguvu na mtu hushtuka katika hali kama vile kapigwa na shoti ya umeme. Hali hii inaweza kupelekea mtu hata kuanguka kitandani na humwamsha mara moja kutoka usingizini.
Wanasayansi wanatuambia kua, pale tu unapopata usingizi kiwango cha upumuaji kinashuka ghafla, mapigo ya moyo nayo taratibu yanapungua, misuli inatulia kwa ku-relax, Kitu cha AJABU hapa ubongo unatafsiri hali hii kama ni DALILI ZA KIFO (brain's misinterpretation of muscle relaxation), hivyo huchukua hatua za haraka za kuushtua mwili kwa kuutetemesha au kuuskuma kwa nguvu, hali ambayo humfanya mtu kuamka kutoka usingizini kwa KURUKA kitu ambacho ni hali isiyo ya kawaida.
Hali hii ikimtokea mtu huambatana na kuongezeka kwa mapigo ya moyo (rapid heartbeat), kuhema haraka haraka, na wakati mwingine mtu hutokwa na jasho jingi.
Wakati mwingine mtu huamka ametoa macho na kama ukimwangalia, nae huishia hukuangalia tu huku akikosa la kukujibu endapo utamuuliza vipi kuna tatizo gani?
MWILI WAKO NI ZAIDI YA UNAVYOUJUA. JAMBO LA MSINGI NI KUONDOA HOFU KWANI MWILI WAKO UNAJUA NINI UFANYE NA WAKATI GANI ILI KUKULINDA USIKU NA MCHANA KATIKA SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO.
9

BAWASILI{HEMORRHOIDS}


Bawasili ni hali ya kuvimba au kutanuka kwa mishipa ya vena{varicose viens} iliopo ndani ya njia ya haja kubwa. Katika ile misuli imara inayozungunguka na kutengeneza muundo wa njia ya haja kubwa pamoja na puru{rectum}ambapo sasa ugawanywa katika aina mbili ya ndani na ya nje.
Bawasili ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi.
Kuna aina mbili za Bawasiri
Nje: Aina hii ya bawasili hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Hali hii huwa na maumivu makali sana na ngoziyake ugeuka kuwa ya blue au zambarau. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina fulan ambalo kitaalamu linaitwa Thrombosed hemorrhoid.
Ndani: Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili.
Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo:
Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.
Je bawasiri husababishwa na nini?
• Tatizo sugu la kuharisha
• Kupata kinyesi kigumu
• Ujauzito
• Uzito kupita kiasi (obesity)
• Kupenda kufanya ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)
• Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.kunyanyua vitu vizito, kikohozi cha muda mrefu nk
• Umri mkubwa,
• Vyakula vya kukoboa,
• Kufanya kazi ukiwa umekaa kwa muda mrefu.
• Kuchuchumaa kwa muda mrefu wakati wa kujisaidia.
• Mtu mwenye tatizo la ini
Dalili za bawasili
• Damu kwenye kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)
• Maumivu au usumbufu njia ya haja kubwa
• Kinyesi kuvuja.
• Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
• Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
• Kujitokeza kwa kinyama (bawasili) wakati wa haja kubwa
Matatizo yanayoweza kutokana na Bawasiri
• Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
• Strangulated hemorrhoids
• Kushindwa kujisaidia kwa amani
Njia za kuzuia Bawasiri
• High fibre diet {makapi lishe}, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.
• Kunywa maji mengi kiasi cha kutosha.
• Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa.
• Fanya mazoezi
Utofauti wa hemorrhoids na rectal fissures
• Bawasili ni hali ya kuvimba kwa mishipa ya vena iliopo ndani ya haja kubwa. Rectal fissures ikiwa ni hali ya kuchanika au kuwa na vidonda kwenye njia ya haja kubwa. Na ikiwa ni tatizo ambali hutokana na kupata kiasi kikubwa kupita uwezo wa njia yenyewe. Hivyo basi kama kutaingia bacteria basi hili huwa ni tatizo la kudumu eneo husika.

MAUMIVU CHINI YA KITOVU KWA WANAWAKE NA WANAUME



TATIZO hili huwakumba watu wengi kwenye jamii lakini kwa bahati mbaya wengi huchukulia ni jambo la kawaida kitu ambacho baadaye husababisha baadhi kuingia kwenye matatizo makubwa ya kiafya hasa kwenye mfumo wa uzazi na mfumo wa chakula.
Maumivu chini ya kitovu hutokea kama ifuatavyo: Yapo yale ya chini ya kitovu katikati, kushoto na kulia. Kwa wanawake maumivu ya kushoto na kulia yapo ya aina mbili.
Kuna yale ambayo yanakuwa upande mmoja lakini husambaa kwa urefu wa sentimita mpaka nne na inaweza ikawa upande mmoja au pande zote mbili lakini yapo mengine chini ya kitovu ambayo yanaweza yakawa upande mmoja au pande zote mbili bila kusambaa kwa urefu.
Kuna maumivu mengine chini ya kitovu huwapata wanawake wakati tu wanaposhiriki tendo la ndoa kwa ndani ya uke au chini ya kitovu. Pia yapo maumivu ambayo huwapata wanawake wakati wameinama, wakati wa kunyanyua vitu vizito, wakati wa kucheka au kuimba na wakati mwingine wakiwa wamelala kifudifudi. Maumivu chini ya kitovu yanaashiria matatizo gani kwa wanawake?
Mirija ya uzazi kujaa maji mazito na machafu ambayo huzuia yai kutembea kwenye mirija ya uzazi. Mwanamke ambaye amewahi kuambiwa na daktari kwamba anatakiwa asafishwe kizazi chake/mirija ya uzazi na wakati huohuo anasikia maumivu chini ya kitovu kushoto na kulia au upande mmoja kuna uwezekano akawa na tatizo la mirija ya uzazi kuziba kutokana na kujaa maji machafu.
Kutokukomaa kwa mayai ya uzazi. Hii husababisha vifuko vya mayai ya uzazi kuvimba (ovaritis) na kumletea mwanamke maumivu chini ya kitovu mithili ya kichomi.
Mwanamke ambaye ana maumivu chini ya kitovu na wakati huohuo ana matatizo ya hedhi, mfano hedhi kukoma au kutokuwa na mpangilio maalum kuna uwezekano mkubwa akawa na tatizo la vifuko vyake vya mayai ya uzazi kutokomaza mayai na hivyo mayai kutotoka kwenye vifuko hivyo na kusababisha kuvimba na hatimaye kumsababishia mwanamke maumivu makali mithili ya kichomi.
Kuvimba kwa kuta za mji wa mimba na kuta za mirija ya uzazi (PID/Pelvic Inflamatory Disease). Mwanamke anayesikia maumivu chini ya kitovu katikati na pembeni kwa wakati mmoja na wakati huohuo akawa anatokwa na uchafu mzito mithili ya maziwa mtindi kuna uwezekano akawa na PID hasa kama amewahi kukumbwa na tatizo la kuharibika kwa mimba kabla haijafikisha miezi mitano.
Afya mbovu ya kibofu cha mkojo ikiambatana na matatizo ya maambukizi kwenye mfumo mzima wa mkojo (UTI). Maumivu chini ya kitovu yanayohusisha afya mbovu ya kibofu cha mkojo huambatana na mgonjwa kutoa haja ndogo kidogo sana ila mara kwa mara.

MATATIZO KATIKA NJIA YA HAJA KUBWA



TATIZO hili huwapata wanaume na wanawake. Matatizo haya hujitokeza katika hali ya tofauti kutegemea na chanzo halisi.
Mfumo wa haja kubwa ni pamoja na mfuko wa kuhifadhia haja kubwa ‘rectum’ na sehemu haja inapokea ‘anus’. Ulaji usiofaa wa vyakula huchangia tatizo hili endapo hupati choo laini mara kwa mara.
Jinsi ya tatizo linavyotokea
Kukosa kupata choo kikubwa mara kwa mara ni mojawapo ya tatizo hili na hii huwapata zaidi watu wanaobadilisha vyakula ghafla kutokana na mazingira, mfano wafungwa, wanafunzi wa bweni na hata ubadilishaji hali ya hewa, mfano unatoka sehemu ya joto unaenda sehemu ya baridi.
Ulaji wa vitu vigumu kama mifupa na miiba ya samaki unaposhindwa kutafuna hutoka hivyohivyo na kukuumiza.
Choo kigumu na kuumia mlango wa haja kubwa husababisha matatizo mbalimbali kama uvimbe, michubuko na nyamanyama kujitokeza.
Inawezekana pia kupata jipu katika njia ya haja kubwa na kukusababishia maumivu makali, michubuko pia inaweza kupata maambukizi na kukufanya uwe na maumivu makali.
Dalili za matatizo
Katika sehemu ya haja kuna kuwa na dalili mbalimbali ambazo kila moja hutibika kivyake na pia inategemea mtu inavyomtokea.
Matatizo ya kufunga kupata choo huwapata pia wazee na wanawake wajawazito na hata waliotoka tu kujifungua.
Mtu anaweza kufunga choo siku zaidi ya tatu na kumsababishia aumwe tumbo chini ya kitovu, kiuno na miguu.
Kufunga choo pia humsababishia mtu kufunga choo na kumfanya ajihisi vibaya, mchovu na hata kuumwa kichwa. Utajikuta unakojoa mkojo wa rangi ya njano sana.
Unaweza kutokwa na kinyama katika njia ya haja kubwa kikiambatana na damu au la, damu hutoka matone matone pale unaposukuma choo kikubwa na hata wakati mwingine kinyama kinatoka na inabidi ukirudishie ndani wakati wa kujisaidia.
Kupata choo kigumu au kuharisha mara kwa mara kunaweza kukusababishia michubuko katika mlango wa haja kubwa na vivimbe vidogovidogo.
 Hali hii inasababisha kinyesi kigande na kupata muwasho hivyo kujikuta unasumbuliwa na muwasho katika njia ya haja kubwa mara kwa mara na kuhisi kama moto.
Endapo hali ya muwasho na maumivu katika njia ya kutokea haja kubwa itaendelea, utajikuta unatoa harufu mbaya ya kinyesi mbele za watu huku nguo zako za ndani zikichafuka.
Hali ya muwasho na maumivu katika mlango wa haja kubwa hukolezwa zaidi endapo utakula pilipili katika mlo wako. Pilipili hupita kama ilivyo katika kinyeshi hivyo kukuumiza katika hiyo michubuko.
Uchunguzi
Uchunguzi wa matatizo haya huendana na dalili halisi za ugonjwa.
Inatakiwa ufanyiwe uchunguzi pale unapohisi maumivu wakati wa kupata haja kubwa, muwasho, uvimbe au hata kufunga kupata choo.
Uchunguzi wa tatizo hili hufanyika katika hospitali za mikoa.
Tiba na ushauri
Pendelea kula matunda na mboga za majani, kunywa maji mara kwa mara na kufanya mazoezi, matatizo yanayojitokeza yatibiwe kama ni kwa upasuaji au kwa kunywa dawa, usile pilipili au kunywa pombe kama
Una matatizo haya.
Mama mjamzito atoe taarifa kwa daktari mara moja kama anafunga choo au ana uvimbe katika njia ya haja kubwa.

MATATIZO YA UZAZI KWA MWANAUME NA JINSI YA KUYAKABILI


Viungo vya uzazi vya mwanaume vimegawanyika katika sehemu kuu mbili. Kuna viungo vya uzazi vya nje na vile vya ndani.
Viungo vya uzazi vya nje ni vile tunavyoviona kama uume na mfuko wa korodani.

Viungo vya uzazi vya ndani ni mirija ya mbegu za kiume ambacho ni kifuko cha akiba cha mbegu na tezi dume au tezi ya ‘Prostate’.
Viungo hivi vyote vina umuhimu mkubwa kwa mwanaume katika kumfanikisha kuweza kufanya tendo la ndoa kwa ufanisi pamoja na uzalishaji wa mbegu za kiume.Matatizo yakitokea katika sehemu yoyote hapo humuathiri mwanaume inategemea wapi athari ipo.
Athari ni kushindwa kufanya tendo la kujamiiana na kuzalisha mbegu au manii. Manii ni majimaji yanayolisha mbegu za kiume na kuzisafisha na huzalishwa na tezi dume.
Chanzo cha tatizo
Hutegemea mahali linapoathirika. Matatizo hutokea popote katika viungo vya uzazi vya mwanaume iwe nje au ndani.
Uume
Matatizo kwenye uume ni kupata maumivu katika njia ya mkojo kutokana na maambukizi au kuumia njia ya mkojo.Mwanaume mwenye tatizo hili hulalamika maumivu wakati wa kukojo, muwasho katika njia ya mkojo na mkojo kutotoka vizuri.
Kuumia kutokana na kuingiziwa mrija wa mkojo mara kwa mara katika njia ya mkojo.
 Maambukizi inaweza kuwa Yutiai za mara kwa mara na magonjwa ya zinaa kama kisonono na mengine.
Ugonjwa wa kaswende huathiri sehemu ya nje ya uume zaidi ambapo vipele na vidonda vyenye muwasho na maumivu  hujitokeza mara kwa mara.Tatizo hili hujitokeza kama tulivyoelezea hapo juu na huchunguzwa katika vituo vya afya.
Ni vema kuwahi hospitali endapo utahisi dalili hizo kwani ukichelewa itasababisha madhara makubwa mojawapo ni kuziba kwa njia ya mkojo, kusambaa kwa maambukizi katika viungo vingine kama kibofu cha mkojo, korodani na tezi dume.Athari nyingine ni ugumba kwa mwanaume.
Tezi dume
Tezi dume ipo kwa ndani jirani na kibofu cha mkojo na mfuko wa haja kubwa. Kazi ya tezi hii ni kutengeneza na kutunza manii.Tezi dume hupatwa na matatizo mbalimbali kama maambukizi na kutanuka hadi kuwa saratani.
Kutanuka huanzia katika umri wa miaka arobaini na tano na huanza taratibu sana.
Maambukizi ya tezi dume hutokana na muendelezo wa maambukizi toka katika njia ya mkojo hadi kwenye kibofu cha mkojo na kufika kwenye tezi dume.
Tezi dume ikitanuka huanza dalili za uhafifu katika utoaji wa mkojo ambapo mkojo hautoki vizuri au unashindwa kabisa kutoka. Tezi hii inapotanuka inabana shingo ya kibofu cha mkojo.
Dalili dhahiri za ugonjwa huu hujitokeza kadiri umri unavyoongezeka, hasa zaidi ya miaka hamsini na sitini.
Endapo utachelewa kupata tiba hadi umri wa zaidi ya miaka sitini, kuna hatari ya tezi hiyo kuwa kansa au saratani.Uchunguzi wa awali wa tezi dume hufanyika kawaida katika  kliniki kubwa kwenye hospitali za mikoa na wilaya kabla dalili hazijajitokeza rasmi.
Kuwa na tabia ya kufanya uchunguzi mara kwa mara hasa unapofikia umri wa miaka 45 na zaidi.  
Kadiri umri unavyoongezeka ndipo dalili zinapojitokeza taratibu hadi tatizo linakuwa kubwa.
Endapo utawahi kufanyiwa uchunguzi mapema , basi tezi dume inaweza kutibika au kuzuia isitanuke na ukaepuka upasuaji na saratani.

MAAMBUKIZI YA TEZI DUME (PROSTATITIS) SEHEMU YA PILI

Maambukizi ya tezi dume bila uwepo wa bakteria (Chronic non-bacterial prostatitis)

Kama jina lake linavyoeleza, maambukizi ya aina hii kwenye tezi dume husababishwa na msongo wa mawazo, matatizo katika vichocheo vya mwili
 (homoni) na hata matatizo katika mfumo mzima wa neva.Pia kumekuwepo na dhana ya kwamba maambukizi ya aina hii huchangiwa na kuwepo kwa

maumivu ya kibofu cha mkojo yanayotokana na maambukizi katika kibofu hicho 
(Cystitis)au hali ya hewa hususan baridi ambayo huongeza maumivu ya tezi dume na hali ya joto ambayo hupunguza maumivu hayo. Baridi pia huchangia kujirudia kwa dalili na viashria vya maambukizi haya.

Katika utafiti uliofanyika kaskazini mwa nchi ya 
Finland (nchi ambayo ina majira ya baridi kali sana),umeonyesha ya kuwepo kwa maambukizi ya aina hii yanayoambatana na dalili na viashiria vyake kali sana kuliko sehemu yoyote duniani.
Maambukizi haya ya tezi dume bila uwepo wa bakteria hutokea kwa wanaume walio katika umri wa miaka 35-45 na inakisiwa kutokea kwa asilimia 90-95 ya maambukizi yote ya tezi dume .

Kuna aina mbili kuu za maambukizi haya ambazo ni:

1.Maambukizi haya yanayoambatana na mcharuko 
(Inflammatory Chronic Prostatitis/Chronic Pelvic Pain Syndrome)
2.Maambukizi yasiyokuwa na mcharuko 
(Non-infalmmatory chronic prostatitis, CP/Chronic Pelvic Pain Syndrome au CPPS)

Nini hasa hutokea wakati wa maambukizi haya?

Kukosekana kwa udhibiti wa mfumo wa neva mwilini kutokana na kuwepo kumbukumbu za maumivu yoyote 
(past trauma), maambukizi kwenye tezi dume, mrundikano wa kemikali tofauti tofauti na kuwepo kwa hali ya kuvutika kwa neva za kwenye nyonga husababisha mcharuko (inflammation) 

katika tezi dume unaosababishwa na kutolewa kwa wingi kwa kemikali aina ya substance P
(kutoka kwenye msihipa ya neva)ambayo ndio husababishwa kutolewa chembechembe zinazosababisha mcharuko mwili (mast cells) kwa wingi na matokeo yake ni kuathiri tezi dume pamoja na viungo vilivyokaribu yake kama kibofu cha mkojo, mpira wa kupitisha mkojo (urethra),korodani nk.

Dalili na viashiria vya maambukizi ya tezi dume bila uwepo wa bakteria
•Maumivu makali ya kwenye sehemu za siri au kwenye nyonga kwa muda wa zaidi ya miezi mitatu bila kuwepo kwa maambukizi ya mfumo wa mkojo 
(UTI)
•Maumivu haya makali yanaweza kuenea hadi kwenye mgongo kwa chini, kwenye puru 
(rectum) na kumfanya mgonjwa kushindwa kukaa chini/ kwenye kiti.
•Maumivu wakati wa kukojoa
•Maumivu katika jointi za mifupa
•Maumivu ya misuli 
(myalgia)
•Maumivu ya tumbo
•Uchovu usioelezeka
•Kichomi kwenye uume/dhakari 
(constant burning pain in the penis)
•Maumivu ya mara kwa mara kwenye nyonga, korodani au kwenye puru 
(rectum) bila uwepo wa maambukizi kwenye kibofu cha mkojo
•Maumivu wakati wa kutoa shahawa (wakati wa kujamiana)
•Kukojoa mara kwa mara
•Maumivu baada ya kutoa shahawa (baada ya kujamiana) ni dalili kubwa ya maambukizi haya
•Kupungua hamu ya kufanya mapenzi
•Kushindwa kujamiana vizuri 
(sexual dysfunction)
•Kushindwa kusimika/kudisa (jogoo kushindwa kupanda mtungi)Erectile dysfuction


Vipimo vya uchunguzi
Hakuna kipimo maalum cha kuchunguza maambukizi haya ya tezi dume.

Vipimo vinavyoweza kusaidia katika uchunguzi wa maambukizi haya ni pamoja na 

•kipimo cha kuangalia shahawa 
(semen analysis)
•kipimo cha kuangalia wingi wa cytokines kutoka kwenye majimaji ya tezi dume
•Vipimo vya kuangalia viashiria vya mcharuko
(inflammation) kama cytokines,myeloperoxidases na chemokines
Inflammatory 
CP/CPPS huambatana na kuwepo kwa seli za usaha (pus cells) kwenye mkojo, shahawa na kwenye majimaji ya tezi dume wakati Non inflammatory CP/CPPS haina seli hizi za usaha kwenye mkojo, shahawa na majimaji ya tezi dume.Kielezo hiki si kigezo cha kutumika kama kipimo cha kuchunguza maambukizi haya.
Seli za usaha (pus cells) huwa ni chembechembe za damu nyeupe zilizokufa.

Matibabu ya maambukizi ya tezi dume bila uwepo wa bakteria
Maambukizi haya sio rahisi kutibu kwani hakuna tiba maalum inayokubalika na wataalamu wa afya.
Lengo kuu la matibabu ya maambukizi haya ni kupunguza mvutano unaosababishwa na kuvutika kwa misuli ya nyonga na ya kwenye puru ,

kupunguza msongo wa mawazo na vichangizi vya msongo huu wa mawazo.

Miongoni wa matibabu yanaweza kusaidia ni pamoja na:
•Kujua chanzo cha msongo wa mawazo/wasiwasi
(panic disorder) au taharuki na kumsaidia mgonjwa kuepuka vichagizi hivi
•Ushauri nasaha pamoja na kumhakikishia mgonjwa ya kwamba hali yake itatengemaa
•Kumuona daktari wa magonjwa ya akili
•Kufanya mazoezi ya yoga ili kufanya nyoga pamoja na mishipa ya neva ya nyoga na misuli kuwa katika hali tulivu
(relaxation)
•Massage ya tezi dume 
(Digital prostate massage)
•Mazoezi ya viungo kwa wale ambao bado hawajafikia hatua ya kupata maumivu makali 
(Chronic Fatigue Syndrome)
•Dawa za kupunguza msongo wa mawazo kama antidepressants, benzodiazipines nk.
•Dawa za antibiotiki na alpha blockers hazijatoa matokeo ya kuridhisha katika uponyaji wa maambukizi haya
•Tiba ya acupuncture imeonyesha kuwapa unafuu baadhi ya wagonjwa

Wanaume wenye maambukizi haya ya tezi dume wako kwenye hatari ya kupata tatizo la maumivu makali sana 
(Chronic fatigue syndrome) na ugonjwa wa Irritable Bowel Syndrome( unaoambatana na maumivu ya tumbo, tumbo kuwa kubwa, kuharisha mara kwa mara au kutopata haja kubwa, msongo wa mawazo, wasiwasi, kuharisha damu na nk)

MAWASILIANO.

MAWASILIANO. SIMU NO. +255 713 684 712 E-MAIL: healthylivingproduct6@gmail.com TUPO : KUNDUCHI BAHARI BEACH