Wednesday, 26 April 2017

TATIZO LA VARICOSE VEINS ( KUVIMBA KWA MISHIPA YA DAMU) WAKATI WA UJA UZITO

Varicose Veins ni tatizo linalowapata baadhi ya wanawake wajawazito. Hili ni tatizo la kuvimba na kuvunjika kwa mishipa ya damu hasa hasa kwenye maeneo ya miguu na mapaja. Pia inaweza kutoka kwenye maeneo ya njia ya haja kubwa(Hemorrhoids/Bawasiri)



Ili kujiepusha na hili tatizo ni vizuri kuongea na wamama na wadada katika ukoo au familia ili kujua kama hili tatizo liko katika familia. Mama mjamzito anabidi ajitahidi kutokustress mwili kwa kutokusimama kwa kipindi mrefu. Kuongezeka kwa msukumo wa damu wakati wa ujauzito unaweka stress kwenye mishipa, hii pamoja na kuongezeka kwa hormone aina ya Progesterone inalegeza misuli ambayo inaweza kusababisha kuvunjika kwa mishipa. Hata kama hukupata hili tatizo wakati wa ujauzito upo uwezekano wa kupata hemorrhoids au vericose veins baada ya kujifungua.

Badala ya kukaa kwenye kitu kwa muda mrefu, jaribu kukaa chini kwenye style ya kihindi yaani tailor sitting.(kama nilivyoelekeza kwenye maada ya mazoezi) Pia jaribu kuweka miguu kuelekea juu/elevated. Fanya zoezi aina la Pelvic rocking. Lala chini huku miguu ikiegemezwa juu ya kochi, kiti au kitanda huku magoti yamekunjwa. Relax katika position hii kwa dakika 10 hadi 15 halafu simama kisha piga piga miguu kwa mikono taratibu.

Fanya mazoezi ya yoga ambayo yanafanya miguu ikae kwa juu, lakini hakikisha una mtaalamu wa kukufundisha jinsi ya kufanya haya mazoezi vizuri. Kuogelea na kutembea pia ni mazoezi mazuri yanayosaidia kukupa mzunguko mzuri wa damu. Unaweza pia kupata massage ya miguu kwa dakika tano kila siku. 

Usivae nguo za kubana, viatu virefu, jizuie kukunja miguu ukikaa, na kukaa kwenye kiti au gari kwa muda mrefu hivi vitu huzuia mzunguko mzuri wa damu

Kula vitungu vya kawaida na vitunguu saumu kila siku. Hivi vinasaidia mishipa ya damu kumaintain elasticity yake.
Vitunguu vya kawaida na vitunguu saumu


Mboga za majani kama bamia  zitasaidia mzunguko mzuri wa damu kwa ujumla. Vyakula vyenye vitamin A, B, C, E vitasaidia kutengeneza kuponya mishipa iliyovunjika.

Usile vyakula vyenye au michuzi yenye pili pili au spices nyingi maana hizi zinaweza kusababisha constipation ambayo inaweza kuzidisha maumivu. Pili pili pia husababisha kutokwa kwa damu katika hii mishipa.

aina ya pili pili zisizotakiwa kuliwa

Pili pili zisizotakiwa kuliwa


Vyakula vya Buckwheat, Oats na Wheat Germ husaidia kuimarisha mzunguko wa damu pamoja na mishipa yake.

Buckwheat
Oats

Wheat Germ

Unaweza kuchukua Beets ukazisaga na kusteam hizi husaidia kusafisha maini na kusaidia usafishaji wa mwili na kupunguza stress kwenye mishipa
Beets

Unaweza ukanywa vitamin E kuzuia na kupunguza hii mishipa iliyovunjika. Mwanamke mjamzito asinywa zaidi ya 600 IU kwa siku kwa usalama wa ujauzito wake
Vidonge vya Vitamin E
Mitishamba mbali mbali itakayosaidia kuponya Varicose Veins:

Chai ya Oatsraw inasaidia kuimarisha mishipa ya damu. Kunywa kikombe kimoja au viwili kwa siku.

Chai ya Oatstraw
 Nettle Tea husaidia kupanuka na kusinya kwa mishipa ya damu kwa ufanisi zaidi. Kikombe kimoja kila siku kuanzia ujauzito mpaka utakaponyonyesha kutasaidia.

Chai ya Nettle
 Majani ya parsley yenyewe au hata chai yake inasaidia sana mishipa ya damu. Changanya kwenye salad au kunywa nusu kikombe cha chai kila siku.

Majani ya Parsley


Chai ya Parsley


Usinywe vinywaji au chai zenye Aloe Vera, Yellow or White Clover kwa sababu hizi husababisha damu kuelekea chini kitu ambacho kitasababisha kuongeza tatizo. Unaweza kunywa chai aina ya red clover badala yake.

Kinywaji cha Aloe Vera Juice usinywe
Chai ya White Clover usinywe
Chai ya red clover unayoweza kunywa
Jinsi ya kuhudumia maumivu yatokanayo na Varicose Veins:

Paka maji ya mtishamba wa Witch Hazel hii itasaidia kupunguza uvimbe na na kukaza mishipa.


Paka maji ya majani ya Comfrey, Yarrow na Mullein itasaidia kupunguza maumivu na kukaza mishipa.
Maji ya Mullein
majani ya mmea wa mullein
Yarrow
mmea wa Yarrow
majani ya Comfrey
Maji ya Comfrey
Safisha mishipa yako kwa maji ya Oak Bark au Apple Cider Vinegar kupungza maumivu
Oak Bark
Maji ya Apple Cider Vinegar

No comments:

Post a Comment

MAWASILIANO.

MAWASILIANO. SIMU NO. +255 713 684 712 E-MAIL: healthylivingproduct6@gmail.com TUPO : KUNDUCHI BAHARI BEACH