Wednesday, 26 April 2017

MATATIZO KATIKA NJIA YA HAJA KUBWA



TATIZO hili huwapata wanaume na wanawake. Matatizo haya hujitokeza katika hali ya tofauti kutegemea na chanzo halisi.
Mfumo wa haja kubwa ni pamoja na mfuko wa kuhifadhia haja kubwa ‘rectum’ na sehemu haja inapokea ‘anus’. Ulaji usiofaa wa vyakula huchangia tatizo hili endapo hupati choo laini mara kwa mara.
Jinsi ya tatizo linavyotokea
Kukosa kupata choo kikubwa mara kwa mara ni mojawapo ya tatizo hili na hii huwapata zaidi watu wanaobadilisha vyakula ghafla kutokana na mazingira, mfano wafungwa, wanafunzi wa bweni na hata ubadilishaji hali ya hewa, mfano unatoka sehemu ya joto unaenda sehemu ya baridi.
Ulaji wa vitu vigumu kama mifupa na miiba ya samaki unaposhindwa kutafuna hutoka hivyohivyo na kukuumiza.
Choo kigumu na kuumia mlango wa haja kubwa husababisha matatizo mbalimbali kama uvimbe, michubuko na nyamanyama kujitokeza.
Inawezekana pia kupata jipu katika njia ya haja kubwa na kukusababishia maumivu makali, michubuko pia inaweza kupata maambukizi na kukufanya uwe na maumivu makali.
Dalili za matatizo
Katika sehemu ya haja kuna kuwa na dalili mbalimbali ambazo kila moja hutibika kivyake na pia inategemea mtu inavyomtokea.
Matatizo ya kufunga kupata choo huwapata pia wazee na wanawake wajawazito na hata waliotoka tu kujifungua.
Mtu anaweza kufunga choo siku zaidi ya tatu na kumsababishia aumwe tumbo chini ya kitovu, kiuno na miguu.
Kufunga choo pia humsababishia mtu kufunga choo na kumfanya ajihisi vibaya, mchovu na hata kuumwa kichwa. Utajikuta unakojoa mkojo wa rangi ya njano sana.
Unaweza kutokwa na kinyama katika njia ya haja kubwa kikiambatana na damu au la, damu hutoka matone matone pale unaposukuma choo kikubwa na hata wakati mwingine kinyama kinatoka na inabidi ukirudishie ndani wakati wa kujisaidia.
Kupata choo kigumu au kuharisha mara kwa mara kunaweza kukusababishia michubuko katika mlango wa haja kubwa na vivimbe vidogovidogo.
 Hali hii inasababisha kinyesi kigande na kupata muwasho hivyo kujikuta unasumbuliwa na muwasho katika njia ya haja kubwa mara kwa mara na kuhisi kama moto.
Endapo hali ya muwasho na maumivu katika njia ya kutokea haja kubwa itaendelea, utajikuta unatoa harufu mbaya ya kinyesi mbele za watu huku nguo zako za ndani zikichafuka.
Hali ya muwasho na maumivu katika mlango wa haja kubwa hukolezwa zaidi endapo utakula pilipili katika mlo wako. Pilipili hupita kama ilivyo katika kinyeshi hivyo kukuumiza katika hiyo michubuko.
Uchunguzi
Uchunguzi wa matatizo haya huendana na dalili halisi za ugonjwa.
Inatakiwa ufanyiwe uchunguzi pale unapohisi maumivu wakati wa kupata haja kubwa, muwasho, uvimbe au hata kufunga kupata choo.
Uchunguzi wa tatizo hili hufanyika katika hospitali za mikoa.
Tiba na ushauri
Pendelea kula matunda na mboga za majani, kunywa maji mara kwa mara na kufanya mazoezi, matatizo yanayojitokeza yatibiwe kama ni kwa upasuaji au kwa kunywa dawa, usile pilipili au kunywa pombe kama
Una matatizo haya.
Mama mjamzito atoe taarifa kwa daktari mara moja kama anafunga choo au ana uvimbe katika njia ya haja kubwa.

No comments:

Post a Comment

MAWASILIANO.

MAWASILIANO. SIMU NO. +255 713 684 712 E-MAIL: healthylivingproduct6@gmail.com TUPO : KUNDUCHI BAHARI BEACH